Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirikisho la Riadha kuhamia Dodoma

7461d56b7172eb7c56499738ecbe124a Shirikisho la Riadha kuhamia Dodoma

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAKAO Makuu ya Ofi si za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) zitahamia Dodoma, imeelezwa. Hatua hiyo ya kuhamishia ofisi hizo Dodoma imefikiwa kwa kauli moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wakati wakifanya marekebisho ya Katiba ya RT, ikiwemo mahali yatakapokuwa makao makuu ya shirikisho hilo la riadha.

Rais wa RT, Anthony Mtaka alisema jana wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jana kuwa baada ya Makao Makuu ya nchi kuhamia rasmi Dodoma, wao (RT), hawana budi nao kuunga mkono hatua hiyo.

Awali, mjumbe mmoja alishauri kwanini makamo makuu ya riadha yasihamie Dodoma, ambako ni katikati ya nchi na itakuwa rahisi kwa kila mkoa kufika Dodoma tofauti na Dar es Salaam.

Aidha, hoja ya kupunguza wajumbe wa mkutano mkuu kutoka watatu hadi mmoja, ndio ilichukua muda mrefu baada ya wajumbe wengi kupinga vikali hatua hiyo, baadhi yao wakidai kuwa watu wataweza kuwahonga wapiga kura wachache ili kupata uongozi RT.

Hatahivyo, kipengele hicho kilitetewa vikali na makamu mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho ya Katiba, Henry Tandau pamoja na Msajili wa Klabu na vyama vya michezo Bara, Ally Mchungahela na hatimaye wajumbe walikubali yaishe kwa kukubali kubaki mjumbe mmoja.

Chanzo: habarileo.co.tz