Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shikalo amtimua kazi kocha Yanga

65882 Pic+shikalo

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KAMA utani, aliyekuwa Kocha wa Makipa wa timu ya taifa ya Vijana U17, Serengeti Boys, Manyika Peter Sr, huenda akatua Jangwani hii ni baada ya kipa mpya wa mabingwa hao wa kihistoria nchini Farouk Shikalo kumfukuzisha mtu kazi Jangwani.Ipo hivi.

Kipa huyo kutoka Kenya, amefichua katika mazungumzo yake na uongozi wa klabu hiyo ameomba kutafutiwa kocha bora mwenye mazoezi ya kisasa na kumbe hilo limeshafanyika kitambo kwa Kocha Manyika baba wa kipa wa KCB, Manyika Peter Jr, aliyewahi kung’ara Jangwani anajiandaa kuja kuchukua nafasi ya mtu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shikalo alisema ame-fanya uchunguzi na kubaini kama atahamia katika kikosi hicho kuna changamoto kubwa ya kocha wa makipa ndio maana akaamua kumweleza ukweli Kocha Mwinyi Zahera alipokutana naye Hispania.

Shikalo alisema akiwa Hispania alipoteta na Zahera ili kumthibitishia anamtaka Jangwani, aliamua kumshtakia jambo hilo baada ya kuwasiliana na makipa wenzake ambao walimfichulia siri hiyo.Kocha wa Makipa wa Yanga kwa misimu kadhaa sasa ni Juma Pondamali ‘Mensah’ ambaye hivi karibuni aliingia kwenye malumbano dhidi ya Klaus Kindoki.

“Nikweli nilimwambia hilo kocha mkuu tukiwa kule Hispania unajua hizo taarifa baada ya kuzisikia nililazimika kuzifanyia kazi sasa niliwasiliana na kipa mmoja ambaye yupo sasa hapo Tanzania akaniambia ni kweli kocha wa makipa Yanga ni changamoto.”“Unajua nililazimika kumwambia Kocha (Zahera) kama ni hivyo ni vyema wakatafuta kocha mwingine haitapendeza kama nitakuja Yanga halafu kiwango changu kikashuka na bahati nzuri kumbe wenyewe wa-likuwa wanalijua na hatua ya kuwaam-bia ilikuwa ni kama kusisitiza tu.

Pia Soma

”MANYIKA ANAKUJA

Katika kulifanyia kazi hilo, kumbe tayari uongozi wa Dk Mshindo Msolla uli-fanya mazungumzo na makocha wawili lakini aliyebakiza hatua moja tu kuchukua nafasi ya Juma Pondamali ni Peter Manyika. Jina jingine ni Razack Ssiwa anayeinoa Bandari Kenya.Yanga imeshafanya mazungumzo ya kina na Manyika na wakati wowote ndiye atakuwa kocha wa kuwapa ubora makipa wa timu hiyo.

Kama Manyika atamali-zana na Yanga ina maana atakuwa na kazi ya kuwanoa makipa watatu, Shikalo, Metacha Mnata na Mkongomani Klause Kindoki.

Chanzo: mwananchi.co.tz