Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shikalo: Huyu Yondani, Yanga ina beki

64820 Yondani+pic

Sat, 29 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIPA wa Bandari anayetakiwa na Yanga, Farouk Shikalo amemuangalia beki Kelvin Yondani kisha akasema jamaa kazi anaijua.

Akizungumza na gazeti hili, Shikalo alisema Yondani ni beki hasa kutokana na akili yake ya kukabiliana na washambuliaji.

Shikalo alisema kama atajiunga na Yanga kisha kucheza pamoja na beki huyo kazi itakuwa nzuri kutokana na uimara wa mkongwe huyo.

Alisema kama isingekuwa uimara wa Yondani, David Mwantika na kipa Aishi Manula, Stars ingepigwa mabao mengi.

Alisema anachopenda kwa Yondani ni utulivu wake na kucheza kwa hesabu kali, mambo yaliyompa ubora katika mchezo huo wa juzi licha ya kupoteza.

“Leo (juzi) ndiyo mara ya kwanza kumuona kwa macho anacheza huyu Yondani (Kelvin) ni beki hodari sana anajua sana nimempenda,” alisema Shikalo.

Pia Soma

“Unajua kipa yeyote kwa beki wa namna ile anayefanya kazi kwa utulivu na akili nyingi, anakuwa na umuhimu sana kwa kipa na ukuta wa timu, na kama isingekuwa hivyo tungewafunga Tanzania mapema sana.”

Chanzo: mwananchi.co.tz