Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shiboub kucheza Ligi kuu Algeria

WhatsApp Image 2020 09 10 At 11.23.10.jpeg?fit=555%2C420 Shiboub kucheza Ligi kuu Algeria

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: dar24.com

Klabu ya Cs Constantine inayoshiriki Ligi kuu nchini Algeria imemsajili aliyekua kiungo wa mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, Sharaf Shiboub kwa mkataba wa miaka miwili.

Shiboub aliachwa na Simba SC, kufuatia mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita, huku sababu nyingine iliyomkosesha dili la kuendelea kukipiga Msimbazi ni kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania Bara mara tatu mfululizo.

Kampuni ya uwakala ya Sifezasports inayofanya kazi na kiungo huyo kutoka nchini Sudan, imethibitisha katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa, Shiboub amejiunga na klabu ya Cs Constantine.

Simba SC waifuata Mtibwa Sugar kwa hasira – Picha“Mteja wetu amekubaliana kujiunga Cs Constatine na hii ni klabu kubwa yenye mtaji wa mashabiki katika Ligi ya Algeria”.

Shiboub na Simba SC kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea katika klabu ya Al Hillal ya nyumbani kwao Sudan.

Chanzo: dar24.com