Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shiboub alivyopotea taifa, Simba ikitolewa kimataifa

Video Archive
Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIUNGO wa Simba aliyeweka rekodi ya kupachika mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza tangu amesajiliwa na klabu hiyo, Sharaf Shiboub ameshindwa kutamba mbele la wapinzani wao UD Songo katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Shiboub aling'ara katika mchezo wa Ngao ya Jamii wakati timu hiyo ikishinda kwa mabao 4-2 alipofunga mabao mawili katika mchezo huo lakini jana Jumapili hakuweza kufurukuta.

Shiboub alitumia dakika 64 na hakuweza kufanya maajabu yoyote ambayo yangeweza kuisaidia timu na kocha, Patrick Aussems aliamua kumtoa na nafasi yake ilichukuliwa na Miraji Athumani.

Msudani huyo alicheza kiungo cha juu akisaidia kusambaza mipira kwa Meddie Kagere na  Clatous Chama aliyecheza namba kumi kutokana na kukosekana na John Bocco ambaye ni majeruhi kwa sasa.

Shiboub alishindwa kuwa mwiba wa wapinzani kutokana na kushindwa kupata msaada ya kiungo ambaye angeweza kufiti kucheza namba sita akajikuta anaingilia majukumu ya wachezaji wengine kama, Jonas Mkude kwa kumsaidia kukaba huku akipanda zaidi kushambulia.

Mkude alishindwa kuwa mchezaji sahihi zaidi katika mchezo huo kutokana na kushindwa kufanya majukumu yake kwa usahihi ya kurudi kuwasaidia Nyoni na Pascal Wawa ambao walijikuta wanasababisha makosa mengi langoni kwao.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz