Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shangwe la Wabunge ushindi wa Simba dhidi ya AS Vita "Simba kushinda ni uchumi wa kati"

Video Archive
Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Mwigulu Nchemba ameliambia Bunge leo Jumamosi Februari 13, 2021 kuwa ushindi wa bao 1-0 walioupata Simba dhidi ya AS Vita unatokana na Tanzania kuwa katika uchumi wa kati.

Mechi kati ya Simba na AS Vita ilipigwa jana katika uwanja wa Martyrs  mjini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikiwa ni mechi yao ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Mwigulu ambaye ni shabiki wa Yanga, watani wakubwa wa Simba, ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha hoja ya mpango wa Serikali aliyoisoma kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

“Hata Simba imeshinda jana kwa sababu Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati kwa hiyo watu wasibeze kuingia hapo maana hatukuomba,”  Mwigulu.

Chanzo: millardayo.com