Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaibu ‘Ninja’ afungiwa mechi tatu

46086 Pic+ninja Shaibu ‘Ninja’ afungiwa mechi tatu

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa Yanga, Abdullah Shaibu 'Ninja' amefungiwa mechi tatu na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kumkuta na hatia ya kumchezea vibaya mchezaji wa Coastal Union.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kamati hiyo imekutana jana Jumapili chini ya Mwenyekiti Wakili Kiomoni Kibamba na kupitia shauri hilo.

Mchezaji Abdallah Shaibu amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 3, 2019, kati ya Yanga na Coastal Union, Shaibu alimpiga kiwiko mchezaji mwenzake alipewa nafasi ya kujitetea.

Ndimbo alisema, Shaibu alikiri kumpiga mwenzake kiwiko wakati wa mchezo baada ya kuonyeshwa video ya tukio na alisema, hakuwa na dhamira ya kufanya kosa hilo alikuwa anajaribu kumzuia asipite baada ya kuona amepiga pasi fupi kwa mchezaji mwenzake.

Kutokana na utetezi wake Ndimbo alisema, Kamati imemtia hatiani, Ninja.

"Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo (zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1) (d) cha Kanuni za Nidhamu TFF," alisema Ndimbo na kufafanua, haki ya kukata rufaa kwa mchezaji huyo iko wazi.



Chanzo: mwananchi.co.tz