Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki wa Yanga alietoka Kigoma kwa miguu akwama Moro kisa tumbo kuumwa (+video)

Video Archive
Wed, 5 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Shabiki wa Yanga Mwanariadha Mang’suli Hussein (45) wa Manispaa ya Kigoma ujiji aliyeamua kukimbia kwa miguu kutoka Kigoma kuanzia April 15 kuelekea Dar es Salaam kutazama Mechi ya Yanga vs Simba mwezi May, amewasili Morogoro usiku wa kuamkia leo lakini amesema anaumwa tumbo na kusema hiyo itamfanya achelewe kufika Dar es salaam.

Tayari ametumia siku 20 tangu aanze safari yake na tarehe ya kufika Dar es Salaam ameibadilisha kutokana na kusumbuliwa na tumbo kwa sasa matarajio yake ni kufika Dar es salaam May 07,2021.

“Niwaombe radhi Watanzania wavute subira kidogo ningekua nimeshaingia Dar es Salaam muda mrefu sasa kutokana na tumbo lilikua linanisumbua siku mbili tatu nikawa nameza dawa tu bila kupima, nimepima leo ikaonekana nina Typhoid kwahiyo kesho nitatumia dawa na Mungu akinijalia Ijumaa nitakua Dar es Salaam kesho nitapumzika, nitaanza safari Alhamisi na Ijumaa May 07,2021 nitakua Dar es Salaam” Mang’suli

Chanzo: millardayo.com