Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki wa Yanga ahamia Simba

50847 Pic+hamia

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

 SHABIKI wa Yanga, Sameer manoty amehamia Simba hivi karibuni kwa madai amechosha na kile ambacho kinaendelea ndani ya klabu ya Wanajangwani. Amesema Yanga ilikuwa na mfadhiri wake na aliyekuwa mwenyekiti, Yusuph Manji ajabu wapo ambao walikuwa wanapiga cha juu kwa manufaa yao na sio timu.

 Kitu kilichomfanya ahamie Simba ni baada ya kuingia kuendesha klabu hiyo kwa mfumo wa hisa ambapo Mo Dweij ndiye mwenyekiti wa bodi ya wadhamini anayemwamini atafanya vitu vikubwa.

 "Nilikuwa Yanga lilialia, baada ya kuona naendelea kuumia na nikifikiria maisha ni mafupi sikutaka kung'ang'ania sehemu ya watu ambao wanataka kujifurahisha kupitia Yanga.

"Sitakaa nihame Simba kwani tayari Mo Dweij ameishaanza kukamilisha Uwanja wa Simba hiki ni kitu kikubwa kwa wapenda soka maana ilianza Azam FC kumiliki uwanja sasa Yanga wanashindwa wapi" alihoji.

Akiwa ndani uzi wa Simba mitaa ya kariakoo na mashabiki wenzake anasema hata watoto wake atawabadilisha wapende klabu hiyo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz