Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki aliyepigwa na Juma Nyosso amezungumza akiwa kitandani Hospitali

1943 Kicg 660x400

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Ni siku ya nne bado Shabani Hussein Kichwabuta anaendelea kuuguza maumivu aliyoyapata siku ya Jumatatu baada ya kupigwa na mchezaji wa Timu ya Kagera Sugar Juma Nyosso mara baada ya mechi yao dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba.

AyoTv na millardayo.com imempata Kichwabuta ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera na kusema kuwa siku ya jana ndo amejitambua na amejikuta yuko hospitalini na kuongeza kuwa hali yake inaendelea vizuri japo kuna baadhi ya maeneo bado ana maumivu.

Aidha amesema Nyoso anamjua vizuri na tabia zake japo hawajawahi kuwa marafiki lakini kipindi cha nyuma waliwahi kucheza wote mpira mchangani jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kitendo hicho kinamfanya awe mwoga wa kuendelea kuangalia mechi.

VIDEO: “BABU SEYA NA PAPII KOCHA SAIVI WAPO STUDIO, WAKO FITI”

Chanzo: millardayo.com