Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawajia juu wasemaji wa klabu

920ab85a42ab40994410acc0747ec570 Serikali yawajia juu wasemaji wa klabu

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imewataka wasemaji wa klabu za michezo nchini kutumia taaluma na maadili katika kutoa matamko na kuacha uropokaji.

Akizungumza na vyombo vya habari Dodoma jana, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alisema wasemaji wa vilabu mbalimbali wamepata mafunzo mara mbili ya namna ya kutoa taarifa badala ya kuwa waropokaji.

“Wasemaji wa klabu wanatakiwa kuzingatia taaluma na maadili wakati wa kutoa taarifa katika klabu zao,” alisisitiza. Dk Abbas alisema wasemaji wa hao wamepata mafunzo mara mbili kati ya Novemba na Desemba, mwaka jana na kati ya Januari na Februari, mwaka huu kuhusu utoaji wa taarifa katika klabu zao, hivyo anategemea kuona mabadiliko.

Alisema kutokana na mafunzo hayo wasemaji wanatakiwa kuhakikisha wanasema mambo mazuri yakiwamo kuhusu klabu zao badala ya kuropoka masuala yanayoweza kuleta vurugu baina ya klabu.

Alisema wasemaji wa klabu wanatakiwa kuzingatia wajibu wao uliopo katika katiba za klabu zao badala ya kutoa taarifa ambazo zinaweza kuhatarisha furaha ya michezo.

Dk Abbas alisema hayo baada ya mwandishi mmoja kueleza kwamba utani wa jadi umegeuka kuwa si utani tena na kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na wasemaji hao kutoa mtamko yao.

Wakati huo huo, Dk Abbas alisema serikali ina mpango wa kuanza kujenga uwanja wa michezo wa kisasa na mkubwa katika jiji la Dodoma.

Alisema bajeti ya ujenzi wa uwanja huo imo kwenye bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo itakayosomwa katika Bunge linaloanza Machi 30, mwaka huu. Dk Abbas alisema michoro ya a uwanja huo tayari imeshakamilika na eneo la kujenga uwanja huo lenye ukubwa wa ekari 230 limeshapatikana mkoani humo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz