Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataja watu nane wanaokwamisha uchaguzi Yanga

32442 Pic+yanga Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo ametaja majina nane ya wanachama ya Yanga wanaodaiwa kuwakwamisha uchaguzi wa Yanga.

Singo alisema Waziri Dk Harrison Mwakyembe tayari ameyapata majina nane ya wanachama wa Yanga ambao wanafanya vikao vya kimya kimya ili kukwamisha uchaguzi huo.

Singo alitaja majina hayo kuwa ni Mustapha Mohammed, Edwin Kaisi, Said Bakari, Shaban Omary, Kitwana Kondo, Boazi Ikupilika, Bakiri Makere na David Sanare.

"Waziri ameweka majina hayo nane hadharani kuwa hao wanakwamisha uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Januari 13," alidai.

"Waziri umeyachukua majina hayo na kuyapeleka katika vyombo husika vya serikali na kama watabainika ni kweli hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

"Waziri alisema hao ambao wanataka kukwamisha uchaguzi ni wale ambao wanapinga ujiudhuru kwa Yusuph Manji na kuna faida ambayo wanaipata kutoka kwa Yanga," alisema Singo.

"Waziri kasema watu hao wakibainika ni kweli wanafanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao," alisema Singo.



Chanzo: mwananchi.co.tz