Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaifungia JKT Tanzania kwa kosa hili

YANAG SCA Serikali yaifungia JKT Tanzania kwa kosa hili

Thu, 18 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imezuia timu ya Jkt Tanzania kucheza na mashabiki uwanjani katika mechi zake zote zilisosalia kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu, kutokana na kukiukwa kwa mwongozo wa Wizara Ya Afya michezoni.

Muongozo huo umekiukwa wakati wa mchezo dhidi ya klabu ya Yanga uliopigwa jana Juni 18, 2020 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Lorietha Lawrence, mashabiki walijazana sana uwanjani hivyo kukiuka kanuni inayoagiza kufuatwa muongozo wa umbali wa mita moja kutoka shabiki mmoja na mwingine.

Aidha taarifa hivyo imesisitiza vilabu wenyeji, wasimamizi wa michezo na wadau wengine kuendelea kusimamia kikamilifu muongozo wa Afya na taratibu nyingine ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live