Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaagiza TBF na BMT kushirikiana

KIKAPU Serikali yaagiza TBF na BMT kushirikiana

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Waziri wa Habari,utamaduni, Sanaa na Mchiezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) kushirikiana kwa karibu na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakikisha kunapatikana mpango mkakati wa pamoja kwa mchezo huo, kwa lengo kuhakikisha mpira wa kikapu

Submitted by George David on Jumatano , 8th Sep , 2021 Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Innocent Bashungwa(Katikati), akiwa na Rais wa TBF, Phares Magesa (Kushoto) na katibu wa BMT Neema Msitha (Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo tarehe 7 Septemba, 2021 alipokutana na viongozi wa TBF pamoja na BMT katika moja ya kumbi za uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam kujadili mwenendo wa mchezo kikapu pamoja na mikakati ya Serikali kuendelea kutoa hamasa katika michezo mbalimbali nchini.

“viongozi wa Shirikisho mnatakiwa kushirikiana kwa karibu na BMT kuhakikisha mnapata mpango mkakati wa pamoja kwa mchezo wa mpira wa kikapu, ili kuhakikisha mpira wa kikapu unaendelea kupiga hatua zaidi kwa ligi za ndani na kimataifa,”amesema Mhe. Bashungwa.

Aidha Mhe. Bashungwa amesisitiza kuwa Wizara yenye dhamana ya michezo itahakikisha inaurekebisha uwanja wa ndani wa Taifa katika viwango vya juu, ili kuendelea kukidhi vigezo vya kuandaa mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa michezo kama vile mpira wa kikapu na wavu.

“niwahakikishie wizara ninayoiongoza itaurekebisha uwanja wetu wa ndani katika viwango vya juu, ili uendelee kukidhi vigezo vya kuandaa mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa michezo yetu inayoyochezwa katika uwanja huo kama vile mpira wa kikapu na wavu,”amesema Mhe. Bashungwa.

 

Chanzo: eatv.tv