Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali na wadau waombwa kuipa thamani Kikapu

UnmTCHED Serikali na wadau waombwa kuipa thamani Kikapu

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mkufunzi wa mchezo kikapu kupitia mpango wake unaojulikana kama Unmatched Basketball, Phineas Kahabi ametoa wito kwa Serikali na wadau wa mchezo huo kujitokeza zaidi ili kuweza kuupa thamani na kukuza kikapu nchi nzima.

Submitted by George David on Jumamosi , 2nd Oct , 2021 Mafunzo ya kikapu kwa wachezaji wenye umri mdogo yanayoendelea Gymkhana, jijini Dar es salaam.

Kocha Kahabi amesema kuwa mchezo wa kikapu ni fursa kubwa kwa vijana wengi wa kitanzania, hivyo amependekeza upewe kipaumbele kwa kutengeneza viwanja vingi zaidi ili kuwapa nafasi vijana kuucheza na kukuza vipaji vyao.

Mchezo wa kikapu umekuwa na hamasa kubwa sana nchini, lakini changamoto ya viwanja imekuwa ikirudisha nyuma juhudu za wachezaji hivyo wadau pamoja Serikali wameombwa kujitokeza kwa wingi, hii ikiwa pamoja na kuandaa mashindano mengi zaidi nchini.

Vile vile Kocha Kahabi amewaomba wadau pamoja na makocha mbali mbali nchini kutengeneza mikakati mingi iwekanavyo ili kufundisha mchezo huo katika ngazi ya awali na kuupa thamani kama wadau wa kwanza wa kikapu.

Chanzo: eatv.tv