Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuifanyia hafla timu ya Olimpiki

Simbu Pic Data Timu ya Riadha iliyoshiriki Michuano ya Olimpiki Tokyo, Japan

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Serikali imeeleza kuifanyia hafla timu ya Olimpiki iliyorejea nchini jioni ya leo ikitokea Tokyo Japan ilipokuwa ikifanyika michezo ya Olimpiki.

Hafla hiyo itaanza kesho saa 12  jioni kwenye hoteli ya Sapphire, Dar es Salaam.

Kaimu Katibu mkuu wa BMT, Neema Msitha amesema hafla hiyo ni ya kuipongeza timu  hiyo ya wanariadha kwa ushiriki wao kwenye Olimpiki.

"Hafla hii itakwenda sambamba na kuiaga timu yetu ya paralimpiki inayokwenda Japan Julai 16 kwenye michezo ya Para Olimpiki," amesema.

Wanariadha wawili wamefuzu kuiwakilisha nchi kwenye Para Olimpiki itakayoanza Agosti 24 jijini Tokyo, Tanzania itashiriki kurusha tufe na kisahani.

Katika Michuano ya Olimpiki iliyoisha wiki iliyopita huko Tokyo,Tanzania ilipeleka wanariadha watatu ambao ni Felix Simbu alieshika nafasi ya 7, Gabriel Geay ambae hakumaliza mbio kutokana na majeruhi na mwanadada Failuna Matanga ambae alishika nafasi ya 24.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz