Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Asilimia 49 za uwekezaji Simba, Yanga si wa mtu mmoja

68080 PIC+SIMBA+YANGA

Wed, 24 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imesema mchakato wa uwekezaji wa klabu za soka nchini kwa kutoa asilimia 49 kwa mwekezaji kuanzia watatu si wa kuhodhiwa na mtu mmoja.

Timu za Simba na Yanga ni miongoni mwa klabu za soka nchini ambazo zimeingia kwenye mchakato wa mfumo wa uendeshaji wa klabu wa hisa.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema mfumo wa hisa unatoa asilimia 49 kwa wawekezaji kuanzia watatu kwenye klabu na asilimia 51 ni za wanachama.

"Hairuhusiwi mwekezaji mmoja kuhodhi asilimia 49, mchakato ulipoanza tuliwambia TFF wasimamie ipasavyo, lakini hawakufanya hivyo.

"Hivyo tumeanza mchakato wa kanuni ya marekebisho na mchakato huo utafanya na BMT na si TFF," alisema Waziri Mwakyembe.

Alisema kamati ndogo ya itaongozwa na mjumbe kutoka BMT, Mkurugenzi ya michezo, TFF, wadau, TRA na soko la mitaji.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz