Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serengeti Boys yatwaa ubingwa wa Ferwafa U17 Kigali 2019

50607 PIC+SERENGETI

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya vijana Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) baada ya sare ya mabao 3-3 na wenyeji, Nyigu Wadogo mjini Kigali jana Alhamisi.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na John Edmund mawili dakika (28 na 49) na Edson Mshirakandi dakika ya 89.

Vijana wa Rwanda mabao yalifungwa na Rutonesha Henson dakika ya 18, Nsanzimfura Keddy dakika ya 20 na Isingizwe Rodrigue dakika ya 94.

Kwa sare hiyo, Serengeti Boys ilimaliza na pointi nyingi zaidi, nne kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Cameroon kwenye mchezo kwanza Aprili 1.

Cameroon imefuatia kwa pointi zake tatu baada ya kuifunga Rwanda 3-1 Machi 29 kwenye mchezo wa kwanza na kwa matokeo hayo wenyeji wameshika mkia kwa kuambulia pointi moja. 

Michuano hiyo ilikuwa matayarisho ya mwisho kwa Serengeti Boys kabla ya kuingia kwenye Fainali za Kombe ka Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, (AFCON U17) katikati ya mwezi ambazo wao ndiyo wenyeji. 

Afcon U17 2019 inatarajiwa kuanza Aprili 14, Tanzania ikianza na Nigeria saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Serengeti Boys itateremka tena uwanjani Aprili 17 kumenyana na Uganda kuanzia saa 1:00 usiku.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz