Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serengeti Boys wakwama kwa Uganda wakifungwa mabao 3-0

52860 Picc+mato

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 imepoteza mechi yake muhimu dhidi ya Uganda baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda mchezo wa fainali za vijana AFcon 2019.

Mabao mawili ya Uganda yaliyofungwa na Andrew Kawooya dakika 15, na Ivan Asaba dakika 27, yametosha kuwatuliza mashabiki.

Bao hilo la tatu la Uganda lililofungwa dakika ya 76, mfungaji alikuwa Najib Yaga.

Mashabiki wengi wa Serengeti Boys waliojitokeza hapa Uwanja wa Taifa kabla ya kufungwa mabao hayo walikuwa aakishangilia muda wote.

Mara baada ya kufungwa mabao hayo mawili walionekana kushangilia kwa sehemu si uwanja mzima kama ilivyokuwa awali.

Mashabiki hao walionekana kuzomea pia pindi mchezaji wa Serengati anapochelewa kutoa au kuaribu pasi.



Chanzo: mwananchi.co.tz