Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serengeti Boys, Cameroon kitaeleweka tu

49542 PIC+CAMEROON

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti Boys tayari iko Rwanda ilikoenda kushiriki michuano maalum ya kirafiki inayoshirikisha timu tatu wakiwamo wenyeji na Cameroon.

Timu hiyo imepanga kuitumia michuano hiyo kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia April 14 hadi 28.

Serengeti Boys iliwasili Rwanda juzi na itaanza kutupa karata yake ya kwanza Jumanne Aprili 2 kwa kuikabili Cameroon na kisha siku mbili baadae itacheza dhidi ya wenyeji Rwanda. Mechi ya ufunguzi ilifanyika jana kati ya wenyeji Rwanda na Cameroon.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Oscar Milambo, amesema watazitumia mechi hizo kama kipimo cha maandalizi yao ya Afcon na anaamini zitawasaidia kuwaweka vizuri wachezaji wake.

“Tumefanya mazoezi kwa bidii kwa muda mfupi na mechi hizi zitatupa picha nzuri ya kitakachotokea Afcon. Tunahitaji kuongeza nguvu katika kufunga mabao.

“Kila eneo tuko vizuri, hivyo kadri tutakavyokuwa tunacheza mechi za kirafiki ndivyo tunagundua wapi tunahitaji kusahihisha makosa na kuongeza nguvu, lakini kubwa zaidi tunataka tuimarike katika ufungaji wa mabao,” alisema Milambo.

Kikosi cha wachezaji wa Serengeti Boys kilichopo Rwanda kina wachezaji 23 ambao ni Jefferson Mwaikambo, Abdallah Mwinyi, Shaban Hassan, Zubery Foba, Pascal Gaudence, Aly Hamis, Ben Anthony, Mohamed Omary, Dominic Pauline, Mustapha Rashid, Morice Michael, Omary Jumanne, Bernard Castory, Agiri Aristide, Edson Jeremia, Tepsi Evance, Charles Herman, Kelvin Pius, Edmund Godfrey, Salum Ally, Arafat Hussein, Boniface Misungwi, Juma Ladaki.

Katika mashindano ya Afcon, Serengeti Boys imepangwa kundi moja na Uganda, Angola na Nigeria wakati Kundi B lina timu za Cameroon, Senegal, Morocco na Guinea.



Chanzo: mwananchi.co.tz