Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senzo awapaisha Manula, Miquissone

Senzo Ed Senzo awapaisha Manula, Miquissone

Mon, 24 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Senzo, ambaye kwa sasa ni Mshauri wa uendeshaji wa klabu ya Yanga, ametoa heshima zote kwa wachezaji aliofanya nao kazi wakati akiwa Simba kutokana na ubora wao katika michuano hiyo ya CAF.

"Heshima zote kwa wachezaji niliofanya nao kazi... kwa kutazama kwa hivi karibuni, Manula [Aishi], Kapombe [Shomary], Luis [Miquissone] na Wawa [Pascal], wameonyesha uwezo mkubwa sana kwenye mashindano ya CAF, wanastahili kucheza klabu kubwa zaidi," aliandika Senzo kupitia mtandao wa Twitter.

Wachezaji hao walikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Saam, dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini timu yao ilitolewa kwa jumla ya mabao 4-3 kutokana na mchezo wa awali kupoteza 4-0 ugenini.

Chanzo: ippmedia.com