Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senzo: Ukitaka mchezaji Simba uwe na uwezo wa kumlipa

84826 Senzo+pic Senzo: Ukitaka mchezaji Simba uwe na uwezo wa kumlipa

Tue, 19 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema wanafikiria kuwatoa baadhi ya wachezaji wao kwa mkopo, changamoto kubwa ni juu ya malipo ya wachezaji hao.

Bosi huyo wa Simba amesema wapo wachezaji wanafikiria kuwatoa kwa mkopo kabla ya kuingiza wapya, lakini hatua ya klabu yao kutakiwa kuendelea kuwalipa imekuwa changamoto kubwa.

Amesema klabu nyingi ambazo zimekuwa zikihitaji huduma ya wachezaji wao zimekuwa zikishindwa kuwalipa mishahara nyota hao na kubaki kuwa jukumu la wekundu hao.

Ameongeza kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwapa ugumu ambapo hatua nzuri kwao kwa klabu yoyote itakayohitaji mchezaji kutoka kwao ni vyema ikamudu kuweza kumlipa kwani wkaati huo haitumikii tena Simba.

Aidha Senzo amesema kwasasa anasubiri ripoti kamili ya kocha wao mkuu kujua idadi ya wachezaji kamili ambao wanaweza kutolewa kwa mkopo ambao watapunguza idadi ya wachezaji wa kikosi hicho.

Simba inataka kukiboresha kikosi chao katika kutumia dirisha dogo la usajili kuingiza mastaa wengine watakarejesha kasi yao katika kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Chanzo: mwananchi.co.tz