Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal warudisha matumaini ya Waafrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia

9585 DgETuynW0AEv4GR TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Timu ya taifa ya Senegal leo imerudisha matumaini ya Waafrika kunako michuano ya kombe la Dunia kwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Poland .



Goli la kwanza la Senegal limepatikana kwa beki wa Poland, Thiago Cionek kujifunga kunako dakika ya 37 huku goli la pili la likitupiwa na Mbaye Niang.

Goli pekee la kufutia machozi la Poland inayoongozwa na Lewandowski likifungwa na Grzegorz Krychowiak kunako dakika ya 86 ya mchezo.

Senegal inakuwa timu ya kwanza kutoka bara la Afrika kupata ushindi kwenye michuano ya kombe la dunia ya mwaka huu nchini Urusi.

Je, Senegal ya mwaka huu inaweza kuvunja rekodi yao ya mwaka 2002 ya kufika robo fainali ya michuano hiyo ya Kombe la dunia? toa maoni yako

Loading...
Chanzo: bongo5.com