Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sasa rasmi masomo ya michezo yarejeshwa vyuo Butimba, Mtwara

C50df41b9d44863e64ca3c36ba3c652f.jpeg Sasa rasmi masomo ya michezo yarejeshwa vyuo Butimba, Mtwara

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Katika kuendelea kuboresha michezo na sanaa nchini, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu kurejesha mafunzo ya michezo katika vyuo vya Butimba na Mtwara.

Amesema wahitimu kutoka vyuo hivyo wataajiriwa kufundisha michezo na sanaa katika shule mbalimbali kwani serikali imejidhatiti kuboresha sekta hizo.

Aidha, ameagiza somo la michezo kwa vitendo kutiliwa mkazo mashuleni na ameiagiza wizara hiyo kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza michezo shuleni.

Amesema kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya, ni muhimu wananchi wakajikita kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vingi kutoka na mfumo wa maisha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz