Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanchez atupia Manchester United

9491 MICHEZO+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miami, Marekani. Alexis Sanchez ametuliza machungu ya kocha Jose Mourinho, baada ya kufunga moja ya mabao katika mchezo dhidi ya Real Madrid.

Bao jingine la Man United lilifungwa na Ander Herrera na kuchangia ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Man United katika mchezo wa kirafiki.

Mshambuliaji huyo alilazimika kusubiri kwa takribani wiki moja kabla ya kupata viza ya kuingia Marekani.

Licha ya kukosa baadhi ya mafunzo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, alicheza kwa kiwango bora mchezo huo ambao Rea Madrid ilipata bao lililofungwa na Karim Benzema.

Man United imepata ushindi wa pili kwa kuviangusha vigogo, baada ya awali kupata ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya AC Milan.

Pia ushindi wa jana umepoza machungu ya kocha Jose Mourinho aliyefura baada ya juzi kunyukwa mabao 4-1 na watani wao wa jadi Liverpool.

Katika hali isiyotarajiwa na wengi, Mourinho alimpanga beki wa kati Eric Bailly katika  mchezo huo. Awali, alisema nyota huyo wa Ivory Coast hana nafasi katika kikosi chake.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz