Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta ataka kumrithi Lukaku Manchester United

61506 SAMATTA+PIC

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema yupo tayari kuchukua kuchukua mikoba ya mshambuliaji Romelu Lukaku wa Manchester United endapo atapata nafasi ya kusajiliwa na miamba hiyo ya Old Trafford.

Samatta baada ya kuisaidia Genk kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu uliopita kwa kufunga mabao 23, ameweka wazi lengo lake ni kucheza Ligi Kuu England.

Akizungumza na runinga ya Azam TV hivi karibuni, Samatta amesema yuko tayari kucheza Manchester United kuziba pengo la Lukaku wa Man United endapo atapata nafasi.

Lukaku amekuwa na wakati mgumu Old Trafford msimu uliopita na amekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kuhamia Inter Milan.

Alipoulizwa na Azam TV endapo anaweza kuvaa viatu vya Lukaku Samatta alijibu: "Kwanini nishindwe? Naweza kuvaa. Mafanikio yanaweza yasiwe kama niliyopata Genk, lakini naweza kucheza, sababu mpira ni uleule. Tayari nipo Ulaya na najua nini natakiwa kufanya kwenye ligi za Ulaya. Itakuwa ni klabu kubwa na presha itaongezeka mara dufu, yaweza kuwa vigumu kuzoea mwanzoni lakini mwisho nitazowea."

Gazeti la The Sun la England jana liliripoti kuwa klabu ya Brighton, Aston Villa zimeingia katika mbio za kumwania Samatta kwa gharama ya pauni 12milioni.

Pia Soma

Brighton, miamba Aston Villa, Leicester, Watford na Burnley zote zimeonyesha nia ya kuitaka saini ya mshambuliaji huyo wa Genk.

Samatta amefunga mabao 23 na kuisaidia Genk kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu huku yeye mwenyewe akitwaa tuzo ya Ebony Shoe inayotolewa kwa mchezaji bora wa Afrika anayecheza Ubelgiji.

Hata hivyo Samatta amekuwa mgumu kueleza ni klabu gani za England anayofanya nayo majadiliano kwa sasa.

Hivi karibuni alidokeza kuwa kuna klabu sita za England zinamuwania.

"Kwa sasa hivi siwezi kusema sana, ni kitu ambacho kipo kwenye mchakato nasubiria kitakapokuwa tayari na wakati utakapofika nitaweza kukizungumza. Lakini sijioni tena Genk, namuomba Mwenyezi Mungu litimie, lakini ikishindikana bado nina mkataba na Genk," alisema Samatta.

Katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari mwaka huu, klabu ya Cardiff ilituma ofa ya Pauni13 milioni kumng'oa Genk, lakini uhamisho huo ukakwama. Hata hivyo Cardiff imeshuka daraja.

Jina la Samatta limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Genk, na wamekuwa wakimuomba mshambuliaji huyo kusalia klabuni hapo kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, klabu hizo ya England inapata ushindani mkali kutoka kwa miamba kadhaa barani Ulaya ziwamo AS Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa.

Chanzo: mwananchi.co.tz