Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta: Tupo Tayari kwa Ajili ya Mchezo wa Equatorial Guinea

Samatta Stars?fit=640%2C360&ssl=1 Samatta: Tupo Tayari kwa Ajili ya Mchezo wa Equatorial Guinea

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Samatta: Tupo Tayari kwa Ajili ya Mchezo wa Equatorial Guinea March 25, 2021 by Global Publishers



MBWANA Samatta, nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Machi 25, 2021 dhidi ya Equatorial Guinea ambao ni maalumu kwa ajili ya kusaka tiketi ya kufuzu AFCON.

Stars chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen iliweka kambi nchini Kenya ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki mmoja dhidi ya Kenya na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Samatta amesema: “Tunatambua kwamba tuna kazi kubwa ya kufanya kusaka ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Equatorial Guinea hilo lipo wazi.

“Ukweli ni kwamba mwalimu ambaye tupo naye anatutambua vizuri kwa kuwa nilifanya naye kazi kwenye timu za vijana na sasa tupo naye kwenye hii timu kubwa ni furaha kwetu.

“Mashabiki wazidi kutuombea dua ili tufanye vizuri nasi tutapambana ili kupata matokeo chanya kila kitu kinawezekana,” amesema.

Chanzo: globalpublishers.co.tz