Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta: Tumewaangusha Watanzania

64724 PIC+SAMATTA

Fri, 28 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NAHODHA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema matokeo waliyoyapata yamewaumiza lakini kibaya zaidi yamewaangusha Watanzania.

Stars inashiriki Fainali za Afcon ambapo imecheza mechi mbili na kupoteza zote ilifungwa na Senegal bao 2-0 na jana imefungwa na Harambee Stars bao 3-2 ambapo imebakiza mechi moja dhidi ya Algeria.

Samatta amesema Stars imepoteza kwa kukosa umakini katika kulinda mabao waliyoyapata wakati wanaongoza mchezo.

Samatta amesema kushindwa kulinda mabao haina maana safu ya ulinzi ya timu yao inapaswa kulaumiwa lakini timu kwa ujumla ndiyo umefanya makosa.

Nahodha huyo amesema  katika kipindi kama hiki cha matokeo mabaya bado umoja unatakiwa kuendelea na sio kushambuliana kwa kuwa hata wao walihitaji kushinda.

Amesema uchanga wao katika mashindano kama haya uliwaghalimu na kushindwa kuhimili kulinda ushindi.

Pia Soma

Samatta amesema hawajakata tamaa na sasa wataangalia jinsi ya kumalizia mchezo ujao dhidi ya Algeria ingawa mechi hiyo nayo itakuwa ngumu.

Chanzo: mwananchi.co.tz