Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakilu avunja rekodi ya Magdalena, Simbu akwama

Alphonce Simbu Sakilu avunja rekodi ya Magdalena, Simbu akwama

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha wa Tanzania Jackline Sakilu ameshika nafasi ya tatu katika mbio za nusu marathoni za Ras Al Khaimah zilizofanyika jana Februari 24, 2024 huko Falme za Kiarabu na kuvunja rekodi iliyowekwa na mwenzake, Magdalena Shauri miaka minne iliyopita.

Katika mbio hizo Sakilu alikimbia kwa muda wa 1:06:04 ambao umemfanya aweke rekodi ya taifa na kuvunja ile iliyowahi kuwekwa na Magdalena Shauri mwaka 2020 ya kukimbia kwa muda wa 01:06:37 katika mbio hizohizo za Ras Al Khaimah.

Mshindi wa kwanza katika mbio hizo ni Tsigie Gebreselama wa Ethiopia akitumia muda wa 01:05:14, huku mshindi wa pili akiwa Muethiopia mwenzake, Ababel Yeshaneh.

Wakenya wanne wameshindwa kufua dafu mbele ya Sakilu ambao ni Margaret Chelimo aliyekamata nafasi ya nne, Evaline Chirchir nafasi ya tano, Catherine Amanangole nafasi ya sita na Peres Jepchirchir aliyekamata nafasi ya saba.

Kwa kuibuka mshindi wa tatu kwenye mbio hizo, Sakilu amejihakikishia kupata Dola 7,000 za Marekani (Sh 17.8 milioni) wakati mshindi wa kwanza akipata Dola 15,000 na wa pili akipata Dola 10,000.

Kwa upande wa wanaume, nafasi tatu za juu tofauti zimekamatwa na Wakenya, Daniel Kibet Mateiko aliyeibuka mshindi, akifuatiwa na John Korir na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Isaia Lasoi huku Mtanzania Felix Simba akishika nafasi ya 10.

Hata hivyo Simbu hajaondoka mikono mitupu kwani amepata kiasi cha Dola 1000 (Sh 2.5 milioni) kwa kumaliza katika nafasi hiyo ya 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live