Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabato afunga bao la mapema zaidi Ligi Kuu Bara

45636 Pic+bao Sabato afunga bao la mapema zaidi Ligi Kuu Bara

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Achana na mjadala unaoendelea kuhusiana na nani ataibuka mfungaji bora msimu huu, je wajua kama Kelvin Sabato ndio mshambuliaji aliyefunga bao la mapema zaidi Ligi Kuu.

Sabato anayechezea Mtibwa Sugar aliyefunga bao la mapema zaidi hadi sasa alifanikiwa kukwamisha mpira nyavuni dakika ya 1 katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika mchezo huo Mtibwa Sugar waliibuka na ushindi wa bao 4-0 mabao mengine yalifungwa na Salum Kihimbwa dakika ya 56, Juma Liuzio dakika ya 63 na Jafari Kibaya dakika ya 90.

Mabao mengine yaliyofungwa dakika ya pili ya mchezo yalikuwa ni mshambuliaji wa Simba, Meddie KagereĀ  alipachika bao lake dakika ya pili.

Nyota wengine waliofunga mabao katika dakika ya pili ni Idd Seleman, Eliud Ambokile Mbeya City kabla ajatimkia nje ya nchi kucheza soka la kulipwa, Ally Shiboli wa Lipuli FC, Mrisho Ngassa wa Yanga, Mohammed Mussa Coastal Union.



Chanzo: mwananchi.co.tz