Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Samatta kutua Leicester

65777 Samatta+pic

Sun, 7 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ubutu wa washambuliaji wa Leicester City, Kelechi Iheanacho na Shinji Okazaki ambaye amesharuhusiwa kuondoka bure klabuni hapo baada ya mkataba wake kumalizika katika kipindi hiki cha uhamisho, ni miongoni mwa sababu zilizoifanya klabu hiyo kuiwania saini ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta.

Leicester City imetenga dau la Pauni 12 milioni ambazo ni sawa na bilioni 34.7 za Kitanzania kama ada ya kuinasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliiwezesha KRC Genk kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Kwa mara ya kwanza, Mei mwaka huu, mabingwa hao wa Ligi Kuu England kwa msimu wa 2015/16 walianza kuhusishwa kuhitaji huduma ya Samatta aliyeifungia Genk mabao 23 kwenye ligi.

Kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers ambaye anainoa Leicester City alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi chake hasa katika idara ya ushambuliaji kutokana na washambuliaji, Iheanacho na Okazaki kushindwa kutoa changamoto ya ushindani kwa Vardy.

Iheanacho ambaye alichwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kutokana na madai ya kocha wake kudai ni mvivu, ameifungia Leicester City bao moja tu katika 30 za Ligi Kuu ya England, japo 21 kati ya hizo aliingia akitokea benchini. Kiujumla Ihienacho ameichezea Leicester mechi 51 za Ligi Kuu na amefunga magoli manne tu.

Upande wa Okazaki ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Japan, licha ya kucheza michezo 24 ya mashindano yote, alishindwa kuifungia bao hata moja Leicester City.

Pia Soma

Vardy ndiye mshambuliaji pekee ambaye alikuwa kama nguzo ya kuegemea kwa Leicester City kwenye safu yao ya ushambuliaji msimu uliopita ambapo aliifungia mabao 18 katika michezo 34 ya Ligi Kuu England.

Mbali na Leicester City, timu nyingine kutoka England zinazowania saini yake ni Aston Villa kwa Pauni 12 milioni, Birmingham (Pauni 11.5 m), Cardiff (Pauni 11 m) na Middlesbrough (Pauni 10 milioni).

Chanzo: mwananchi.co.tz