Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Azam FC kumkataa refa Nkongo kuwachezesha

1962 Screen Shot 2018 01 25 At 11.04.30 PM 660x400.png

Fri, 26 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Uongozi wa Azam FC leo January 25 2018 umeandika barua rasmi kwenda Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) inayoelekea kutokuwa na imani na mwamuzi Israel Nkongo.

Mwamuzi huyo ndiye amepangwa kuchezesha mchezo ujao wa Azam FC dhidi ya Yanga, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi January 27 2018 saa 10.00 jioni.

“Kama klabu, itakumbukwa kuwa mechi zetu ambazo mwamuzi huyu (Nkongo) amekuwa akizichezesha zimekuwa na malalamiko mengi na utata mwingi juu ya maamuzi ya uwanjani,” ilisema moja ya nukuu kwenye barua hiyo.

Refa Israel Nkongo aliyeshika mpira pichani.

Barua hiyo ilizidi kueleza kuwa moja ya sababu nyingine ya kumlalamikia mwamuzi huyo na kukosa imani naye, ni kitendo chake cha kuzua utata mkubwa kwenye mchezo aliochezesha mkoani Mbeya wiki moja iliyopita kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City kutokana na uamuzi wake.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, aliyeandika barua hiyo na kutuma nakala kwa Kamati ya Waamuzi, TFF na Yanga, ameweka wazi kuwa kwa kuzingatia uzito wa mchezo huo wameiomba bodi hiyo kubadilisha mwamuzi kwa kumpanga mwingine.

Aidha katika barua hiyo, Mohamed ameongeza kuwa kutokana na timu zote mbili kutoka katika mkoa wa Dar es Salaam, ameiomba bodi hiyo kumpanga mwamuzi ambaye atatoka nje ya mkoa huo.

Mbali na Nkongo kupangwa kuchezesha mchezo huo, waamuzi wengine waliopangwa kushirikiana naye ni Josephat Bulali atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, msaidizi namba mbili atakuwa Soud Lila, mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii huku Omar Abdulkadir akiwa Kamishna wa mchezo huo, wote wakitoka Dar es Salaam.

CHANZO: azamfc.co.tz

Msimamo wa Kagera Sugar baada Nyosso kutoka kwa dhamana

Chanzo: millardayo.com