Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saba wapewa jukumu kuisimamia Yanga

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Wadhamini la Yanga limeunda kamati ndogo itakayosimamia mechi za timu hiyo huku pia wakiunda kamati kamili ya kusimamia mchakato wa uchaguzi .

Akitangaza maamuzi hayo jana Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini George Mkuchika alisema kamati hiyo itakayokuwa na watu saba chini ya mwenyekiti Lucas Mashauri itakuwa na jukumu la kusimamia timu yao katika mechi zilizosalia mpaka watakapopatikana viongozi wapya katika Uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Aprili 28.

Mkuchika ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais Utawala Bora aliwataja wajumbe wengine ni pamoja na Said Ntimizi atakayekuwa makamu mwenyekiti wajumbe wakiwa Hussein Ndama,Moses Katabaro,Maulid Kitenge,Hussein Nyika na Samuel Lukumay.

Akifafanua juu ya kuwarudisha Lukumay na Nyika Mkuchika alisema wao kama Baraza la Wadhamini wanaiheshimu ufanisi uliofanywa na wajumbe hao ambao mapema jana walijiuzulu nafasi zao za ujumbe wa kamati ya utendaji na kwamba uzoefu wao umewapa nafasi ya kurudishwa kufuatia timu yao kutotetereka wakishirikiana na wenzao wawili Siza Lyimo na Thobias Lingalangala ambao walishajiuzulu wiki chache zilizopita.

"Kamati hii naomba nieleweke hatujaunda kamati ya kuendesha timu(interim) hiyo inakatazwa na Fifa sisi tumeunda kamati ya kusimamia timu kwamba itaondokaje kwenda kucheza mpira watalala wapi lakini mambo ya uendeshaji yapo chini ya sekretarieti.

" Kamati hii sasa tunaamini itatusaidia kuisimamia vyema timu yetu iendelee na kufanya vizuri.

Aidha Mkuchika alitangaza kamati ya uchaguzi itakayokuwa chini ya mwanasheria mkongwe Sam Mapande.

Mbali na Mapande wengine ni Daniel mlelwa,mustapha Nagali,Godfrey Mapunda,Edward mwakingwe,Samuel mangesho,issa gavu,venance mwamoto,seif gulamali na dastan kitandula



Chanzo: mwananchi.co.tz