Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SIMBA YATOLEWA NJE NA AL AHLY YAELEKEA VITAL’O FC YA BURUNDI

Haji Manara Simba 23042017 1tv3xsrgkxzun103ryj2tg89sv?fit=800%2C445 SIMBA YATOLEWA NJE NA AL AHLY YAELEKEA VITAL’O FC YA BURUNDI

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Leo Agosti 19 /2020 Klabu ya Simba imetangaza timu itakayocheza nayo katika Siku ya Simba Day ambayo itakua ni tarehe 22 /2020, ambapo mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Mkapa Jijini Dare es Salaam.

Manara amesema kuwa walipanga kucheza na Al Ahly “Tulipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tunaamini Vital’O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo.”

“Vital’O itafika ijumaa saa 5 asubuhi na jioni timu zote zitafanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkapa”– Haji Manara.

“Uwanja wa Uhuru kutakuwa na big screen na wachezaji na benchi la ufundi wakifika wataenda kwanza kule kusalimia.”

Simba Day inatarajiwa kupambwa na burudani mbali mbali na kwa upande wa Siku ya Kesho Alhamisi Simba imesema itakuwa na BIG SURPRISE kwa Wanasimba MC atakuwa Mpoki.

Storyr na www.dimbani.co.tz

Chanzo: zanzibar24.co.tz