Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SIMBA WAVUNJA KAMBI RASMI

Aaeeec8c4066066836c5dc31a9f32ba5 SIMBA WAVUNJA KAMBI RASMI

Wed, 28 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATAWALA wa soka la Tanzania Bara Simba jana wamevunja kambi rasmi baada ya kikosi chao kuwasili Dar es Salaamu kikitokea Kigoma, ambapo Jumapili kilitwaa taji la Kombe la FA na kukamilisha idadi ya mataji matatu msimu huu.

Simba ilianza kutimiza malengo yao kwa kubeba Ngao ya Jamii kwa kuifunga Namungo FC mabao 2-1, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kisha wakafanikiwa kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa msimu wa nne mfululizo kabla ya Jumapili kukamilisha taji la tatu la Kombe la FA kwa kuwafunga watani zao Yanga bao 1-0 mchezo ukipigwa Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kambi yao imevunjwa mara baada ya timu kuwasili Dar es Salaam na wanatarajiwa kukutana tena baada ya wiki mbili kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao.

Kiongozi huyo alisema kwa sasa wanasubiria kupata taarifa ya kuanza kwa kambi rasmi kutoka kwa kocha wao Didier Gomes pamoja na uongozi wa wa juu wa Simba, sababu maandalizi yao yanatakiwa kuwahi kuanza kutokana na mipango iliyopo ya kwenda kupiga kambi nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya wa ligi na michunao ya kimataifa.

Akizungumzia ubingwa wao wa Kombe la FA, Rweyemamu alisema ulikuwa mchezo mgumu kwao na wapinzani wao pia, lakini anafurahi kuona wamepata ubingwa huo kwa kuwafunga watani zao Yanga ambao waliwapa ushindani mkubwa hadi dakika ya mwisho ya mchezo.

Nacho kikosi cha Yanga kiliwasili jana Dar es Salaam kikitokea Kigoma.

Chanzo: www.habarileo.co.tz