Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SIMBA SPORTS CLUB Inaliamsha Afrika keshokutwa

28938 Simba+pic TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ligi ya mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho inaanza kesho na keshokutwa kwa timu mbalimbali kushuka dimbani.

Simba na JKU zinacheza Ligi ya Mabingwa wakati Mtibwa Sugar na Zimamoto zenyewe zitakuwa na kibarua Kombe la Shirikisho Afrika.

Tukiiangazia Simba, inaingia ikiwa na hesabu kali za kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kauli ya kocha

Akizungumzia maandalizi yake, anasema hakuna kitu kikubwa kitakachobadilika kwani hata mchezo wao na Lipuli walitoka suluhu kwa kuwa akili nyingi ilikuwa katika mchezo wa Mbabane.

“Muda mwingi wachezaji tumewajenga kwenye saikolojia ya Afrika sasa ilikuwa ngumu kubadilika ndio maana mchezo na Lipuli ulikuwa mgumu kwetu, lakini walipambana.

“Wachezaji walikuwa na fikra za mechi ya Jumatano na ilikuwa bahati kwenda vyumba vya kubadilishia nguo tukiwa suluhu.

Hata hivyo, Aussems alikataa kuzungumzia mchezo huo akasema: “Ngoja kwanza nifanikiwe kupita ndio nitakwambia, lakini kama hatutofanikiwa basi nitakwambia pia kwamba haikuwa droo nzuri kwetu kwahiyo vuta subira.”

“Ninachokisema kwa sasa ni kwamba tumewaandaa wachezaji kusahihisha makosa ya Lipuli, kuwatengeneza washambuliaji na kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumatano.

“Mechi ya Lipuli imetuamsha na tutaifunga tu Mbabane mashabiki wasiwe na wasiwasi,” anasema Aussems.

Mchezo wa kwanza utachezwa keshokutwa Jumatano Novemba 28 na marudiano ugenini kati ya Desemba 4 na 5 mwaka huu.

Mshindi wa Jumla wa mechi hiyo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Nkana Red Devils ya Zambia na UD Do Songo ya Msumbiji kusaka timu itakayofuzu hatua ya

Katika mashindano hayo pia JKU ya Zanzibar itaanzia nyumbani itakapoivaa Al Hilal ya Sudan na mshindi wa jumla wa mechi hiyo atakutana na mshindi wa mechi baina ya APR ya Rwanda na Club Africain ya Tunisia.

Kwenye Kombe la Shirikisho Mtibwa Sugar itakutana na Northern Dynamo ya Shelisheli na mshindi wa mechi hiyo atacheza na KCCA ya Uganda wakati Zimamoto ya Zanzibar itacheza na Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

Endapo Zimamoto itashinda mchezo huo watakutana na mshindi wa mechi kati ya El Geco ya Madagascar na Deportivo Unidado ya Guinea ya Ikweta kuingia kwenye makundi.

Mbabane hawa hapa

Mbabane Swallos si ngeni Tanzania kwani iliitupa nje Azam katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika katika raundi ya kwanza mapema mwaka 2017.

Kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Swaziland ikiwa imecheza mechi 10, ikishinda sita, sare moja na imepoteza mechi tatu.

Mafanikio

Ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara saba. 1993, 2005, 2009, 2012, 2013, 2017 na 2018 lakini ikatwaa Kombe la FA kwa mwaka 1986, 2006, 2013, 2016.

Mabingwa hao pia waliibuka mabingwa wa Swazi Charity Cup mwaka 1993, 1999, 2004, 2014, 2017 na 2018.Kombe la Ligi; 1997, 1999, 2007, 2016, 2017, 2018 wakati ubingwa wa Swazi top 8 Cup walitwaa mwaka 2013, 2015, 2016 na kombe la PLS Ultimate walitwaa mwaka 2012

Pia walitwaa Ubingwa wa King Mswati III Cup mwaka 2015 na pia walikuwa mabingwa wa Mbabane Mayoral Cup (Town Century celebration) makwa 2002.

Kimsingi, Mbabane hawana maajabu makubwa kwenye mashindano ya klabu Afrika. Mara kadhaa wamekuwa wakitoka raundi ya awali au raundi ya kwanza.

Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo iliingia mara sita, na mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1998 waliaga hatua ya awali sawa na 2006, 2010, 2014, 2015 na mwaka 2018 iko hatua za awali.

Kombe la Shirikisho zamani Kombe la CAF, 1994 ilitoka raundi ya awali wakati mwaka 1995 raundi ya kwanza lakini 1987 ilitolewa raundi ya awali.

Kikosi

Kikosi cha timu hiyo kinaundwa na wachezaji wengi wanaocheza nyumbani, isipokuwa wachezaji nane wanatoka mataifa mbalimbali Afrika.

Wachezaji hao ni viungo; Kingu Yallet (DR Congo), Richard Sewu (Ghana) na Siphamandla Matsenjwa kutoka Afrika Kusini.

Pia kiungo mkabaji Gabriel Goshen (DR Congo) na mashambuliaji Jean Claude Amougou kutoka Cameroon. Wengine ni winga Phathizwe Sacolo (Afrika Kusini), mshambuliaji wa kati Sallieu Tarawallie (Sierra Leone), Daniel Atakorah (Ghana) na Quadri Kola Aladeokun kutoka Nigeria.



Chanzo: mwananchi.co.tz