Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"SIJAFURAHISHWA NA SAKATA LA MORRISON NA YANGA" - Mwakyembe

Mwakyembe Waziri?fit=730%2C395 "SIJAFURAHISHWA NA SAKATA LA MORRISON NA YANGA" - Mwakyembe

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Sakata la mchezaji Bernard Morrison bado limeendelea kuwepo kweye vichwa vya habari ambapo usiku wa jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amesema hajafurahishwa na mgogoro wa mchezaji huyo na Yanga kwasababu limeleta changamoto kwa Baraza la Michezo la Taifa.

Waziri Mwakyembe amesema suala hilo limeingilia sera za michezo ya nchi na kuwapa fundisho la kuangalia upya katika hizo timu mbili za Simba na Yanga, ili waone kama  zinapoleta wachezaji ziruhusiwe kupokonyana ili soka lisije kuvurugika.

”Hebu tuangalie hasa hizi timu mbili (Simba na Yanga) zinapoleta wachezaji, je ziruhusiwe kunyang’anyana wachezaji hapa hapa, kama mchezaji anaondoka kwenye timu aondoke kwanza kisha atoke huko aombe kurudi tena huku sio hapahapa itatuletea matatizo’‘amesema Dr. Mwakyembe.

Aidha Mwakyembe amesema kwasasa hawezi kuingilia suala hilo kwani sio la kisera na kwamba TFF na wadau wengine wa soka watalimaliza na wakishindwa wanaelewa ni jinsi gani watalileta kiserikali.

”nimepokea taarifa ya kutoka kwa Rais wa CAF Ahmad Ahmad, akisema hajawahi kuona ushindani wenye hamasa kubwa katika soka kama wa timu mbili za Tanzania jambo ambalo linaleta heshima kwa nchi yetu”

Chanzo: zanzibar24.co.tz