Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TFF

717a433eea3b67b8f44145e03615d733 SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TFF

Thu, 24 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema serikali itashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) katika kuendeleza michezo.

Bashungwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipofanya kikao na shirikisho hilo akiwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Abdallah Ulega na kusema ni lazima serikali na shirikisho hilo kuwa na mpango mkakati wa pamoja wa kuendesha michezo nchini.

“Serikali tuko tayari kushirikiana na TFF, hivyo lazima shughuli zote za michezo za timu za taifa za ndani na nje ya nchi serikali iwe na taarifa” alisema Bashungwa.

Aliongeza kuwa shirikisho hilo lazima liweke kipaumbele kwenye michezo ya watoto wa shule za msingi na sekondari ili kupata wachezaji wazuri wa timu za Taifa.

“Nasisitiza utawala bora katika kuendesha michezo ikiwemo usimamizi madhubuti wa fedha zinazoingia TFF” alisema Waziri Bashungwa.

Naye Naibu Abdallah Ulega alisisitiza kuwa shirikisho hilo lisimamie mchango wa soka katika kupata fedha za kuhudumia timu za Taifa.

“Ni lazima tuzo kwa wanamichezo zirejee na zipewe uzito unaostahili, lengo ni kutambua mchango wa wanamichezo katika Taifa letu” alisema Ulega Alisisitiza kuwa TFF isimamie klabu vinavyoshiriki Kombe la Mapinduzi zipeleke timu bora kwa heshima ya kombe hilo.

Naye, Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia alisema wameanza kutekeleza ilani ikiwemo kuwa na mpango mkakati wa kuendeleza michezo pamoja na kuimarisha utawala bora.

Chanzo: habarileo.co.tz