Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SEIF ‘TIOTE’ AIVUSHA SALAMA KVZ FAINALI YA FA CUP, KVZ YAKUSANYA KIJIJI

Image 321.png?fit=566%2C377 SEIF ‘TIOTE’ AIVUSHA SALAMA KVZ FAINALI YA FA CUP, KVZ YAKUSANYA KIJIJI

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mchezaji wa kikosi cha Kvz Seif Said Tiote ameivusha salama timu yake katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuipatia ushindi wa goli moja huku wapinzani wao Uhamiaji walitoka bila matokeo yeyote mfukoni.

Uhamiaji kipindi cha kwanza iliitawala mchezo na ndipo mchezaji Seif Tiote akaona aipatie timu yake goli la mapema na ndio goli hilo pekee Kvz ndilo lililowapa ushindi mbele ya Uhamiaji.

Kvz itaelekea Kisiwani Pemba kwajili ya kucheza fainali ya mwisho ambapo atakutana na mshindi atakaepatikana Leo kati ya Tekeleza au New Star na mchezo huo utapigwa katika Dimba la Gombani Agosti 22/2020

Kvz ilikusanya kijiji kwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki uwanjani hapo huku wapinzani wa Uhamiaji walienda na mashabiki wao kiasi.

Chanzo: zanzibar24.co.tz