Fainali za Kombe la Dunia zimeanza huko Russia na zinaendelea, leo ni siku ya Kundi G japo kuna mechi moja ya Kundi F.
Mechi ya Kundi F, Sweden itacheza na Korea Kusini itakayochezwa kwenye Uwanja wa Nizhny Novgorod kuanzia saa 9:00 alasiri.
Lakini mechi ya kukatana shoka itakuwa kati ya wawakilishi wa Afrika, Tunisia dhidi ya England kwenye Uwanja wa Volgograd nayo ikianza saa 9:00 alasiri. Mpambano mwingine leo utakuwa kati ya Ubelgiji itakayokwaana na Panama lakini mechi hii ikichezwa kwenye Uwanja wa Sochi kuanzia saa 12:00 jioni.
Mechi zinaendelea, lakini huku nje ya uwanja, kumetolewa tangazo la kibaguzi kwa wale watakaokwenda kushuhuduia fainali za Kombe la Dunia hasa watu weusi. Tamara Pletnyova, mkuu wa masualaya bunge (familia) alisema Kamati ya Wanawake na Watoto ya Russia imewaonya wananchi za Russiakutojihusisha kimapenzi na mashabiki ama watu watakaokuja kwa ajili ya fainali hizi. Zaidi wameonywa wanawake wa Russia kutofanya mapenzi na wageni kwani inaweza kuwa kama ilivyokuwa Michezo ya 1980 ya Olimpiki kule Moscow.
“Kuna wasichana watakaokutana na wanaume, na matokeo yake watawapa mimba,” Pletnyova alisema: “Labda wakubaliane kuoana, na inawezekana hawatafanya hivyo. Sasa hapo watakaohangaika ni watoto, ambao walihaha kama ilivyokuwa Michezo ya Olimpiki ya Moscow.”
“Tangu kipindi hicho cha Soviet, watoto ndoo walikuwa wakihangaika.” (Kama ukifanya mapenzi, usijaribu kuchanganya rangi
Lakini Pletnyova alitahadharisha zaidi kwamba ikiwa mambo yatakwenda kama watu wanavyotaka, kutakuwa na watoto kibao nje ya ndoa.
Warusi wameshawatahadharisha wanawake wao kuwa wasitembee na watu weusi na kama wakishindwa kabisa watambee na watu weusi ili watoto watakaopatikana wawe wazungu. “Kama ni mtu wa jamii tofauti na mweupe, itakuwa mbaya zaidi,” Pletnyova alisema. “Lazima watoto wapatikane wenye asili yetu.”
Russia ina asilimia kubwa ya ubaguzi wa rangi hasa katika viwanja vya michezo na hii si mara ya kwanza kwa matukio kama haya kutokea Russia.
FIFA iliwahi kuitoza faini Russia Dola30,000 kwa mashabiki kuwafananisha wachezaji weusi sawa na kima wakati wa mashindano ya Mabara mapema Mei.
Mchezaji wa England, Danny Rose amewaambia wanafamilia yake kubakia hotelini muda mwingi kwa kuhofia masuala ya ubaguzi wa rangi. Hata hivyo, Russia imeahidi kuuzima ubaguzi.
Danny Rose, ambaye ni mwanasoka mweusi wa England, aliiambia Evening
“Kwa mimi sina shaka, lakini nimewaambia wasiwe wanatoka, watadhihakiwa. Kwa mimi sina shaka, ninaiangalia familia yangu.