Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rooney ageukia Masumbwi, kuzipiga na Jake Paul

Rooney X Jake Paul Rooney ageukia Masumbwi, kuzipiga na Jake Paul

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Promota wa ngumi za kulipwa nchini Uingereza, Eddie Hearn ameweka wazi kuwa Legend wa Manchester United, Wayne Rooney amemtumia ujumbe wa kuomba pambano na mara kadhaa amekuwa akihitaji kuingia ulingoni kuzipiga na Jake Paul.

Rooney ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa DC United inayoshiriki Major League Soccer (MLS) amezungumza na promota huyo kuhusu mtazamo wake wa kuingia ulingoni siku zijazo.

Akizungumza na That Peter Crouch Podcast, Hearn amedai ''Wayne anapokuwa amekunywa, atanitumia ujumbe na kuanza kusema nitapigana naye, nitapigana naye.''

Eddie Hearn ameahidi kutimiza pambano hilo na huwenda likawa la kihistoria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live