Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo na Messi wauaga mwaka kwa style ya kipekee (Picha)

927 47B0189400000578 5227271 Image A 32 1514854850899 TZW

Tue, 2 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Wachezaji bora zaidi duniani, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kila mmoja amesherehekea sikukuu ya mwaka mpya kwa staili ya haina yake.

Ronaldo ameonekana akitupia picha katika mtandao wake akiwa amezungukwa na tuzo zake 15 ambazo amewahi kuzinyakua toka kuanza kucheza soka la kulipwa akiwa katika ardhi ya nyumbani kwao huko Madeira.

Wakati kwa upande wa Messi, yeye ameuwaga mwaka 2017 kwa kutupia picha akiwa na mke wake, Antonella Roccuzzo ambae anatarajia kupata mtoto wa tatu.

Kwa mujibu wa meneja wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde anaamini kuwa Lionel Messi ndiye mchezaji bora zaidi duniani.

Messi mwenye umri wa miaka 30, goli lake la mwisho amelifunga katika mchezo wake dhidi ya Real Madrid Uwanja wa Santiago Bernabeu kabla ya Christmas.

Messi ameshinda mabao 22  katika michezo  29 aliyocheza ndani ya klabu na timu yake ya taifa msimu huu.

Chanzo: bongo5.com