Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo moto unawaka, Juve na Bayern zafuzu 16 bora UEFA

UCL UEFA  0 Ronaldo moto unawaka, Juve na Bayern zafuzu 16 bora UEFA

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: eatv

Michezo ya mzunguko wanne michuano ya klabu bingwa barani Ulaya iliendelea tena usiku wa jana kwa michezo nane kutoka makundi manne, miwili ikipigwa mapema saa 2:45 usiku na mingine sita ilichezwa kuanzia saa 5:00 usiku.

Kutoka kundi G, Wolfsburg ya Ujerumani ilipata ushindi wake wa kwanza wa michuano hiyo msimu huu kwa kuifunga timu ngumu ya Austria ambao ni vinara wa kundi hilo kwa 2-1 wakati Mabingwa watetezi, Chelsea wakiifunga Malmo 1-0.

Michezo sita iliyoendelea kuanzia saa 5:00 usiku ni ule uliokuwa unafuatiliwa na wengi, Atalanta ikilazimishwa sare kenye uwanja wake wa nyumbani 2-2 na Manchester United kwa mabao 2 ya Cristiano Ronaldo dakika 45+1 na 90+1.

Mabao hayo yanamfanya CR7 kurekodi bao lake la 6 kwenye michezo 4 ya makundi ya michuano hiyo huku akiweka rekodi ya kuhusika kwenye mabao 179 kwenye michezo 180 kwenye michuano hiyo tokea alipoanza kuichezea.

Mabao mawili hayo pia yamemfanya afikishe mabao 139 na kuendelea kutanua akaunti yake ya mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo kuliko mchezaji yeyote kwenye historia ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kutoka Kundi E, Wababe wa Ujerumani, Bayern Munich waliwasha moto na kuifunga Benifica ya Ureno 5-2 huku mshambuliaji wake Robert Lewandowski akifunga Hat Trick kwenye mchezo wake wa 100 kwenye michuano hiyo.

Juventus ya Italia kutoka kundi H, iliwanyuka watakatifu wa Urusi, Zenit St. Petersbough 4-2 huku Paul Dybala akiingia kambani mara mbili na kutoa assist moja na kuonesha kiwango safi kilichozidi kuwaweka kileleni mwa kundi hilo.

Bayern Munich na Juventus ndiye timu mbili pekee zilizoshinda michezo yake 4 ya mwanzo na kuwa na ushindi wa 100% hivyo kuwa timu pekee zilizofuzu hatua inayofuata ya mtoano 16 bora zikiwa na michezo miwili mkononi.

Matokeo mengine ni: Kundi E: Dynamo Kyiv 0-1 Barcelona, Kundi F: Villarreal 2-0 Young Boys, Kundi G: Seville 1-2 Lille.

Chanzo: eatv