Cristiano Ronaldo" /> Cristiano Ronaldo"/> Cristiano Ronaldo"/>

Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo hakamatiki, avunja rekodi ya muhenga Seedorf na Andres Iniesta barani Ulaya

8401 DeME9alVAAEa Lr TZW

Mon, 28 May 2018 Chanzo: bongo5.com

height="400" class="wp-caption-text">Cristiano Ronaldo

Kwa ushindi wa jana wa klabu yake dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa barani Ulaya unamfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza barani Ulaya kuwahi kutokea kuchukua kombe la Klabu Bingwa mara tano.

Ronaldo amewaacha wakongwe wawili, Andrés Iniesta ambaye amechukua mara nne akiwa na Barcelona na kiungo wa zamani wa klabu ya AC Milan, Clarence Clyde Seedorf waliokuwa naye pamoja kwa kuchukua kombe hilo mara nne.

Miaka ya Iniesta aliyochukua Kombe la UEFA akiwa na Barcelona

2005/06 (Barcelona)

2008/09 (Barcelona)

2010/11 (Barcelona)

2014/15 (Barcelona)

Miaka ya Seedorf aliyochukua kombe la UEFA akiwa na klabu tatu tofauti tofauti.

1994/95 (Ajax)

1997/98 (Real Madrid)

2002/03 (Milan)

2006/07 (Milan)

Ronaldo amechukua mara tano akiwa na klabu mbili, Manchester United mwaka 2007/08 huku akichukua mara tano akiwa na Real Madrid.

Japo Messi, Gerard Pique na Xavi Hernandez wamechukua mara nne lakini kuna fainali moja hawakucheza uwanjani tofauti na Ronaldo ambaye yeye kwenye fainali zote alizoshinda taji hilo amecheza.

Xavi Hernández: 2006*, 2009, 2011, 2015 (Barcelona)

Lionel Messi: 2006*, 2009, 2011, 2015 (Barcelona)

Gerard Piqué: 2008*, 2009, 2011, 2015 (Manchester United, Barcelona)

*Ni miaka ambayo wachezaji hao hawakucheza kwenye michezo ya fainali wakati Barcelona ilipoibuka mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya.

Loading...
Chanzo: bongo5.com