Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ajibia suala la mfuata Messi Ufaransa

JOSE FONTE CR7 Ronaldo ajibia suala la mfuata Messi Ufaransa

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Nahodha wa mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa, klabu ya Lille, beki kitasa Jose Fonte amesema amekuwa akimtumia ujumbe nahodha wake wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ili atue kwa mabingwa hao na kuwapiku PSG kwenye mbio za ubingwa wa ligi kwa misimu ijayo.

Jose amefunguka hayo usiku wa jana baada ya kuulizwa kuhusu ujio wa Lionel Messi aliyethibitishwa kutua kwa matajiri kwa jiji la Paris, klabu ya PSG kwa kandarasi ya miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Barcelona ya Hispania.

Jose Fonte aamesema, “Nimekuwa nikimtumia ujumbe Cristiano kuja kujiunga na Lille kila siku lakini, jibu lake ni kicheko tu, ha ha ha”. 

Jose ambaye ni miongoni mwa walinzi wa kati wenye umri mkubwa kwenye ligi hiyo akiwa na mika 37 ameonekana kutishika na ujio wa Messi kwa kukiri kuwa safu ya ushambuliaji ya PSG itakuwa na makali zaidi na kuwawia vigumu sana wao walinzi na wapinzani kiujumla kuwakabiri.

“Ni jambo zuri hususani kwenye suala la ushindani. Itakuwa hata ngumu zaidi kwetu lakini, tupo tayari kwa changamoto hiyo”. Vuta picha umefanikiwa kucheza bila kuruhusu goli dhidi ya Messi, Neymar na Mbappe! Ni utatu wenye makali sana. Ushindani wa ligi mwaka huu utakuwa wakuvutia sana”.

Fonte pia alionekana kushangazwa na namna utarataibu wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA unavyofanya kazi kuhusu kuthibiti mapato na matumizi ya vilabu yaani 'Financial Fair Play' kutokana na kuendelea kuona matajiri hao wa Ufaransa kusajili wachezaji mastaa zaidi wenye mishahara mikubwa.

“Nataka nigusie eneo lengine, japo nataka kuelewa suala la 'Financial Fair Play' nchini Ufaransa. Kila klabu inadhibiti matumizi yake. Hawawezi kununua sana, hawawezi kulipa wachezaji mishahara mikubwa lakini PSG wanafanya kana kwamba sheria hii haipo”.

“Ni kitu kizuri Ligi kuu ya Ufaransa kuwa na Leo Messi lakini, ki kawaida unapaswa kuangalia eneo lenigne, je ni uungwana huu?. Kila mtu anathibiti bajeti yake hapa Lille, wachezaji baadhi wamepaswa kupunguza mishahara yao”.

“Alafu PSG unamuona Gianluigi Donnarumma anasajiliwa, Sergio Ramos anasajiliwa, unamuona Georginio Wijnaldum anasajiliwa...wachezaji wote hawa wanakuja na mishahara mikubwa na tayari wana wachezaji wengi wenye mishahara mikubwa tayari. Na hapa ndipo kujiuliza kwingi kunako kuja”. Alimalizia hivyo, Jose Fonte.

PSG inahaha kutafuta uwiano mzuri wa kimahesabu katika vitabu vyao kwa kukiri kuwaweka sokoni wachezaji wake kumi ili kukabiriana na 'Financial Fair Play'.

Chanzo: eatv.tv