Straika wa zamani wa Brazil na Barcelona Ronaldinho ametangaza kustaafu uchezaji wa soka.
kwa mujibu wa wakala wake Roberto Assis ambaye pia ni kaka wa mchezaji huyo ametangaza rasmi kwamba mchezaji huyo amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 37.
Ronaldinho hakuwa na klabu ya kitaalamu tangu kuondoka Fluminense ya Brazil mwaka 2015.
Assis amesema kwamba kustaafu kwa Ronaldinho kutaacha alama na tukio la kombe la dunia litakalo fanyika nchini Urusi mwezi Juni mwaka huu.
“He’s quit football, it’s over. Let’s now do something nice, big as it should be, after the Russia World Cup, maybe in August,” Assis aliliambia O Globo
Wakala huyo aliongezea kwa kusema kwamba watafanya baadhi ya matukio mbalimbali ya kisoka katika nchi mbalimbali ikiwemo Brazil, Ulaya na Asia. Na wameshaanza kupanga baadhi ya mikakati na timu ya Taifa ya Brazil.
Ronaldinho alifanya mambo muhimu ikiwemo kunyakua Kombe la Dunia mwaka 2002, Ligi ya Mabingwa mwaka 2006 na tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2005.
Na Raheem Rajuu