Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robinson agomea chanjo, augua Covid-19

ROBINSON CALLUM Robinson agomea chanjo, augua Covid-19

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Westbromwich Albion, Callum Robinson ameefunguka na kusema licha ya kuugua Covid-19 mara mbili lakini bado ameamua kukaa bila kuchanja kwa sasa mpaka hapo atakavyo fikiria tofauti.

Robinson aliuugua ugonjwa huo kwa mara ya kwanza Novemba 2020 kabla ya chanjo kushika hatamu, lakini aliugua tena Agosti mwaka huu wa 2021 kipindi ambacho chanjo zilishaanza kutumika ikiwemo nchini kwa Jamhuri ya Ireland.

Akijibia kama atachanja baada ya kuugua mara mbili Robinson mwenye miaka 25 amesema, “Sijapata chanjo, Hapana. Huo ndiyo uamuzi wangu kwa sasa. Inanisumbua kwamba niumwa mara mbili lakini sijachanja, huenda nikabadilisha mawazo huko mbele”. Amesema Robinson.

Robinson ni miongoni mwa wachezaji walioipa makali Westbrom kwenye Championship kwa kucheza michezo 11 na kukusanya alama 22 utofauti wa alama 3 na Kinara klabu ya Bournemouth.

Chanzo: eatv.tv