Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Riadha yatoa cheti kwa wadau

Mita 200000000000000000000000 Riadha yatoa cheti kwa wadau

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Timu hiyo itashiriki michezo ya Olimpiki nchini Japan kuanzia Julai 23 hadi Agosti 8, 2021, ambapo timu itaondoka Julai 29 hadi Nagai, Japan kupiga kambi kabla ya kwenda Tokyo kushiriki michezo hiyo.

Miongoni mwa wadau waliokabidhiwa cheti ni kampuni ya Silent Ocean, ambayo imesaidia timu hiyo vyakula vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 3 kwa ajili ya wanariadha waliopo kambini wakiendelea kujifua.

Akitoa cheti hicho jijini Dar es Salaam juzi, Rais wa RT, Silas Isangi, aliishukuru Silent Ocean na kusema imekuwa mstari wa mbele kusaidia mchezo wa riadha na hasa timu ya taifa inayojiandaa kwa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

"Tutahakikisha msaada unaotolewa na Silent Ocean kwa ajili ya timu iliyopo kambini, unatumika vizuri kwa malengo yaliyopangiwa ili kuleta maendeleo katika mchezo huo," alisema Isangi.

Naye mwakilishi wa Silent Ocean, Mohamed Kamilagwa, alisema, wameamua kuusaidia mchezo huo kwa kuwa watu wengi hawako mstari wa mbele kusaidia, licha ya kuliletea sifa kubwa Tanzania kupitia kina Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui na wengineo.

"Mchezo wa riadha umeliletea taifa letu sifa kubwa kuliko mchezo mwingine wowote kupitia kwa magwiji hao na wengineo, lakini hawapati udhamini unaostahili na ndio maana sisi tumeamua kuwasaidia," alisema Kamilagwa.

Alisema wataendelea kuusaidia mchezo huo na kama hali ya janga la virusi vya corona litatulia, basi wanatarajia kuipeleka China timu ya taifa ya riadha kwa ajili ya kambi ya muda mrefu.

Mratibu wa misaada hiyo, Nelson Mrashani, alisema, amekuwa akifanikisha kupatikana kwa misaada baada ya kuridhika na jitihada zinazofanywa na uongozi mpya wa RT wa kuuendeleza mchezo huo. 

Chanzo: ippmedia.com