Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Riadha Arusha: Magufuli alitufundisha uzalendo

Ec5537e6c1622f5a064e60c834bc4b01.jpeg Riadha Arusha: Magufuli alitufundisha uzalendo

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIONGOZI wa mchezo wa riadha mkoani Arusha wameeleza kumkumbuka na kutambua mchango wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli aliyekuwa misimamo thabiti na mzalendo wa kweli kwa taifa.

Akizungumza jijiji hapa jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday alisema michezo ni kielelezo cha uzalendo na utaifa na kwamba Magufuli alipenda Afrika itambulike kama Afrika.

"Magufuli aliahidi kwamba atajenga uwanja mkubwa wa michezo mkoani Dodoma ambao utakuwa na michezo yote, kilio chetu na matumaini yetu tulifarijika baada ya kusikia hotuba nzuri ya Rais wa sasa Mama Samia Suluhu kuwa tusitazame mbele kwa wasiwasi maana ametuhakikishia yale maono yote yatayatekelezwa chini yake,” alisema Gidabuday.

Alisema misimamo ya Magufuli katika kufuata taratibu, sheria na haki ndio umewezesha wanamichezo kuishinda medali na ili kumuenzi, wanamichezo wanamichezo wanatakiwa kufuata haki na taratibu.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), Rogath Steven alieleza kuwa watamkumbuka Magufuli kwa mambo ya msingi hasa wakati dunia ikiwa 'Lockdown' yeye alisema wanamichezo waendelee na mazoezi yao na hiyo ilisaidia kujiandaa vyema na wanariadha wa Tanzania walivyoenda katika mashindano walifanya vyema.

"Tutamkumbuka kwani alikuwa akiwapa wanamichezo motisha, kitendo hicho pia kinatufundisha kuwa wazalendo zaidi," alisema Steven.

Alisema Chama cha Riadha Mkoa Arusha kinatoa pole kwa serikali, familia ya Dk John Magufuli na Watanzania wote na kwamba wanaungana na wananchi wote katika msiba huu wa taifa.

"Sisi tuliobaki twende katika mfumo ule ule ambao Magufuli aliokuwa akitaka," alisema Steven.

Chanzo: www.habarileo.co.tz