Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi zaibeba Simba kwa Mwadui, Kagere kuendeleza moto wake

82318 Pic+simba Rekodi zaibeba Simba kwa Mwadui, Kagere kuendeleza moto wake

Wed, 30 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba inajivunia rekodi yake nzuri wakati inapoivaa Mwadui leo kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Simba inajivunia rekodi yake ya kushinda mechi tano dhidi ya Mwadui tangu ilipopanda Ligi Kuu Tanzania msimu wa 2015-16.

Simba imefungwa mara moja kwenye Uwanja wa Kambarage na Mwadui huku timu hizo zikitoka sare mara mbili katika michezo nane waliyokutana hadi sasa.

Vinara wa Ligi Kuu, Simba wanakwenda katika mchezo huo wakiwa wameshinda mechi zote na kukusanya pointi 18 na kufunga mabao 12 na kufungwa mawili.

Wenyeji Mwadui ikiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi nane imeshinda moja na kudroo tano, wakifungwa mbili, huku wakifunga mabao sita na kufungwa saba.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella alisema kwa anavyoiona Simba haoni nafasi ya Mwadui kuwazuia leo. "Simba wanakikosi kipana ambacho kina kila mchezaji bora kulinganisha na wale wa Mwadui kwahiyo nawapa nafasi kushinda leo, ingawa mpira una matokeo ya kushangaza pia," alisema Mogella.

Walipokutana mara ya mwisho msimu uliopita kwenye kwanza Uwanja wa Kambarage, Simba ilishinda 3-1, mabao yaliyofungwa na John Bocco mawili na Meddie Kagere. 

Katika mchezo huo Bocco alimpiga ngumu beki wa Mwadui, Revocatus Mgunga na kupewa kadi nyekundi.

Mechi ya pili iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda tena mabao 3-0 dhidi ya Mwadui ambayo yalifungwa na Bocco, Kagere na Mzamiru Yassin.

Msimu wa 2017-18, mechi ya kwanza Simba wakiwa nyumbani walishinda mabao 3-0, na ule wa marudiano ulimalizika kwa sare 2-2.

Wakati msimu wa 2016-17, Mwadui mechi ya kwanza wakiwa nyumbani walifungwa mabao 3-0, na Simba huku mechi ya pili walifungwa tena 2-1 katika uwanja wa Taifa.

Msimu wa kwanza ambao Mwadui walipanda kucheza ligi ilikuwa 2015-16, ndio walifanikiwa kupata matokeo mazuri kwa maana mechi ya kwanza Taifa walitoka sare ya 1-1, wakati mchezo wa pili Simba walikubali kulala kwa kufungwa 1-0.

Chanzo: mwananchi.co.tz